Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa winga 'legendary' Mrisho Khalfan Ngasa, mmoja wa wachezaji walioipa heshima kubwa klabu ya Yanga
Ngasa hakuwahi kuficha mapenzi yake kwa Yanga hata katika nyakati alizokuwa akizitumikia klabu nyingine
Akiwa na Yanga Ngasa amefanya mambo makubwa, amewahi kuwa mfungaji bora ligi ya mabingwa lakini pia bado anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye timu ya Taifa akiwa na mabao 25
Huyu ni mchezaji ambaye ataendelea kubaki mioyoni mwa mashabiki na hakika jina lake litaendelea kubaki katika vitabu vya kumbukumbu pale Jangwani
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu kwake
HAPPY BIRTHDAY NGASA
ADVERTISE HERE