Yanga Princess leo imekamilisha michezo ya viporo ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya TSS Queens
Clara Luvanga amechukua mikoba iliyoachwa na Aisha Masaka ambaye leo ameelekea Sweden kucheza soka la kulipwa katika moja ya timu za Ligi Kuu
Luvanga amefunga mabao matano leo, akifikisha mabao 11 katika michezo mitatu iliyopita
Yanga Princess imesogea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Wanawake baada ya kufikisha alama 26
wako nyuma ya vinara Simba Queens kwa tofauti ya alama saba
Bado kuna michezo 11 katika duru ya pili
ADVERTISE HERE