Wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, kampuni ya NBC kwa kushirikiana na TFF, leo wamezindua Bima kwa ajili ya wachezaji zaidi ya 600 wa ligi kuu
Bima hiyo maalum itamuhusu mchezaji, baba, mama na watoto wawili
Bima hiyo itamsaidia mchezaji kupata matibabu ndani au nje ya nchi pale inapobidi
Hii ni hatua muhimu kuhakikisha afya za wachezaji zinalindwa
Endapo mhusika akipata ugonjwa wa kudumu utakaomzuia kucheza mpira au kuhudumu katika timu yake, fao lake litakuwa kati ya Tsh milioni tatu (3) hadi milioni 30
Ikitokea mchezaji amepata ulemavu wa kudumu utokanao na ajali au majanga, fao lake litakuwa kati ya Tsh. Milioni 10 hadi 100
Endapo itatokea kifo kwa mhusika kutokana na ajali au maradhi mengine fao lake ni kati ya Tsh. milioni 10 hadi 100 ambapo fao litatolewa kwa familia ya mhusika.