Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara ametamba kuwa hakuna klabu ya Tanzania inayoweza kumsajili mchezaji yeyote wa Yanga
Manara alikuwa akikanusha tetesi zinazodai kuwa Simba inawanyemelea baadhi ya nyota wa klabu ya Yanga
Manara amesema kwa sasa Yanga ina kila kitu, zaidi inawavutia wachezaji wa timu nyingine kujiunga nayo
"Hakuna klabu yoyote ambayo inaweza kumsajili mchezaji yeyote kutoka Yanga nataka nikuhakikishie, tuna kila kitu"
"Hawana ubavu huo na wasijaribu kutuchokoza kwani tunajua huko kwao kuna wachezaji 11 wanamaliza mikataba na wanatamani kujiunga na nasi," alitamba Manara huku akiwatahadharisha Simba Sc
"Wao wanafahamu nini kilitaka kutokea msimu uliopita, wanafahamu nilifanya kazi kubwa kutuliza mambo, wasituchokoze..!"
ADVERTISE HERE