Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi pamoja na benchi lake la ufundi wamefanya kazi kubwa kuboresha viwango vya wachezaji na kutengeneza timu imara sana
Zipo nyakati Yanga inawakosa wachezaji muhimu ambao wamekuwa wakichangia mabao mengi lakini bado Wananchi wameendelea kutakata
Walishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold ugenini katika mchezo mgumu ambao wengi waliamini Yanga ingedondosha alama
Jana wamecheza na KMC wakiwakosa nyota wao muhimu kama Khalid Aucho, Saido Ntibazonkiza na Jesus Moloko lakini bado Wananchi wameendelea kuuwasha moto
Sasa Yanga inashinda sio kwa sababu ya mchezaji mmoja mmoja, inashinda kwa sababu ya timu
Yeyote anaweza kukosekana lakini 'mentality' ya ushindi inabaki kwenye kikosi
Nabi amewafanya wachezaji wajiamini sana, angalia umahiri anaoonyesha Farid Mussa kule upande wa kushoto akiwa mlinzi
Hakuna aliyetarajia kuwa Farid anaweza kuwa mlinzi mahiri, Nabi amemuamini na mwenyewe akajiamini na sasa anachofanya kitabaki kuwa historia
Muangalie Salum Abubakar 'Sure Boy' katika eneo la kiungo. Kuna walioamini Yanga inapomkosa Aucho inakosa umahiri katika eneo la kiungo, lakini sio kweli
Yannick Bangala ameendelea kudhihirisha anaweza kuwa usajili bora uliofanywa na Yanga baada ya Fiston Mayele
Feisal, Nkane, Mayele, Djuma, Job, Mwamnyeto na Djigui Diarra wameendelea kuipa thamani Yanga katika kila mechi
Huu mota wa Wananchi haitakuwa kazi rahisi kuuzima!