Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi klabu ya Yanga Dominic Albinus ametoa ufafanuzi kuhusu idadi ya kadi za njano ambazo amepata kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' kuelekea mchezo dhidi ya KMC
Albinus maarufu Baba Paroko amesema taarifa sahihi ni kuwa Sure Boy ana kadi mbili tu za njano alizopewa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Geita Gold
"Nimepokea maswali mengi kuhusu kadi za njano za Sure Boy, ukweli ni kwamba anazo kadi mbili tu alizopata katika michezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Geita Gold," amefafanua Albinus
Yanga inashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili KMC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
ADVERTISE HERE