Wananchi wana jambo lao katika dimba la Benjamin Mkapa baadae leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku
Ni siku ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salima Suluhu Hassan, Yanga imeandaa burudani 'kibao' pale uwanja wa Benjamin Mkapa kunogesha siku hii kabla ya mchezo dhidi ya KMC
Hautakuwa mchezo mwepesi, zinapokutana Yanga na KMC ushindani haukosekani. Yanga imekuwa na mwenendu mzuri wa matokeo, ushindi utawahakikishia kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi katika msimu ambao Wananchi wana kiu ya ubingwa
KMC wameimarika ukinganisha na walivyoanza msimu huu, wametoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union kwa kufungwa mabao 3-2, hivyo ni wazi watajaribu kujilinda ili wasipoteze mchezo wa pili mfululizo
Ni bahati mbaya kwao Wanakutana na Yanga ambayo ni ya 'moto' kwelikweli licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kama Salum Abubakari 'Sure Boy' mwenye kadi tatu za njano, Khalid Aucho, Saido Ntibazonkiza na Jesus Moloko ambao ni majeruhi
Yanga imepata ahueni baada ya idadi ya majeruhi kupungua kwani wachezaji Kibwana Shomari, David Bryson, Farid Mussa, Juma Shabani na Chico Ushindi wote wako tayari kwa mchezo huo
Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kuhakikisha wanapata ushindi ili kuongeza gep la pointi dhidi ya watani zao Simba kuwa 11