Mambo muhimu kuelekea uchaguzi wa Matawi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Mar 2022
Mambo muhimu kuelekea uchaguzi wa Matawi Yanga

Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama klabu ya Yanga Simon Patrick amefafanua masuala kadhaa muhimu kuelekea uchaguzi wa Matawi unaotarajia kufanyika kuanzia March 18 mpaka mwishoni mwa mwezi April 2022

Haya hapa mambo muhimu ya kuzingatia;

1. Kila tawi lazima lichague Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Wajube 4 hii ni kwa mujibu wa ibara ya 62(3) ya Katiba ya Yanga.

2. Gharama za kugombea nafasi hizo ni Tsh. 30,000/= kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, Tsh. 20,000/= nafasi ya Katibu na Katibu Msaidizi, Tsh. 30,000/= kwa nafasi ya Mweka Hazina na Tsh. 15,000/= kwa nafasi za wajumbe, hela hizi zitalipwa kwenye tawi husika na zitabaki kwenye tawi kwa matumizi ya tawi.

3. Kila tawi litawakilishwa na watu 5 kwenye Mkutano Mkuu ambao ni Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na wajumbe 2 (mmoja lazima awe mwanamke kama yupo) hii ni kwamujibu wa ibara ya 17(1) ya Katiba ya Yanga.

4. Matawi yote nchini yanatakiwa kuanza mchakato wa uchaguzi kuanzia tarehe 18/03/2022 mpaka 30/04/2022 ambapo kila tawi linatakiwa kuwa limetuma orodha ya Viongozi wote waliochaguliwa kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu.

5. Matawi yatakayo tambuliwa na kupata uwakilishi kwenye mkutano mkuu ni yale tu yaliokidhi sifa ya kuwa na Wanachama zaidi ya 100+ kwa matawi ya ndani ya nchi na Wanachama 20+ kwa matawi ya nje ya nchi hii ni kwa mujibu wa ibara ya 62 (1) ya Katiba ya Yanga.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’