Kocha Mkuu wa Yanga, Nasriddine Nabi amesema endapo watapata ushindi katika mechi tano zijazo za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, basi wataanza kuufikiria ubingwa.
Yanga ina pointi 45 baada ya kucheza mechi 17 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 37
Mechi tano zijazo za Yanga ni dhidi ya KMC, ambayo itachezwa Uwanja wa Mkapa Machi 16, Azam FC Aprili 6, Azam Complex, Simba Aprili 30, Ruvu Shooting Mei 4 na Namungo FC Mei 8 mechi zote tatu za mwisho zitapigwa Uwanja wa Mkapa.
Kocha huyo mwenye uraia pacha wa nchi za Tunisia na Ubelgiji, amesema michezo hiyo ni miongoni mwa michezo migumu iliyoshikilia hatima yao ya ubingwa.
"Siyo kwamba tunazihofia timu hizo, hapana bali ni mechi ambazo zina presha kubwa kutokana na mazoea yalivyojengeka, lakini baadhi yao zina malengo ya ubingwa kwa hiyo hazitokuwa mechi rahisi, lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,"alisema Nabi
Nabi amesema wanachokifanya yeye na wachezaji wake ni kuweka bidii katika kila mchezo ambao upo mbele yao na sasa kutofikiria ubingwa sababu kazi waliyoianza bado haijamalizika