Ametetema tena huko Mwanza katika uwanja wa CCM kirumba! Ni Fiston Kalala Mayele akifunga bao lake la 10 msimu huu na kuwaangamiza Geita Gold katika uwanja wao wa nyumbani
Linaweza kuwa moja ya magoli ya mapema sana yaliyofungwa msimu huu akiweka kambani bao kwenye sekunde ya 30 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Geita Gold
Dhamira ya Yanga kuhitaji ushindi katika mchezo huo ilionekana mapema tu, baada ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha kuanza mchezo
Haukuwa mchezo mwepesi kwani Geita Gold wamedhihirisha wako imara pengine kama sio uzoefu wa wachezaji wa Yanga, mambo yangekuwa tofauti
Ushindi muhimu kwa Wananchi ambao wanaendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 45, alama 11 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili
Ndio! waambieni ni alama 11 tena! Wengi leo walikuwa upande wa Geita wakiamini Wananchi hawatapata alama tatu
Mchezo unaofuata ni dhidi ya KMC utapigwa March 16 uwanja wa Benjamin Mkapa




