Miongoni mwa sababu zinazoipa Yanga jeuri ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu pengine pasipo kupoteza mchezo ni pamoja na mpangilio wa ratiba yake
Mashabiki wa Yanga waliumia sana baada ya timu yao kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika katika hatua ya awali kabisa kwa kufungwa na Rivers United
Lakini pengine kama Yanga ingeweza kutinga makundi, isingekuwa na matokeo ambayo wameyapata mpaka sasa
Ni kwa sababu robo tatu ya wachezaji walikuwa wageni na hivyo kocha Nasreddine Nabi alihitaji muda kuwaunganisha
Kwa kuwa Yanga haina michuano ya Kimataifa, imenufaika na mpangilio wa ratiba kwa kupata muda mrefu wa kujiandaa
Nabi amepata muda mzuri wa kukiimarisha kikosi chake na hakuna shaka msimu ujao Yanga haitapata usumbufu kushiriki michuano ya Kimataifa kwani mpaka sasa tayari inanufaika na upana wa kikosi chake
Katika michezo kadhaa iliyopita, Yanga imewakosa takribani wachezaji nane kutokana na majeraha na sababu nyingine lakini makali ya timu yamebaki vilevile
Michezo miwili imesalia kukamilisha mwezi wa tatu ambapo baada ya mchezo dhidi ya Geita Gold March 06, mchezo utakaofuata utapigwa dhidi ya KMC, March 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa