Wananchi uwanjani dhidi ya Kagera Sugar leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2022
Wananchi uwanjani dhidi ya Kagera Sugar leo

Kikosi cha Yanga leo kinaendelea na msako wa ubingwa  wa ligi kuu msimu huu wakiwakaribisha Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa moja usiku

Baada ya kumaliza kibabe duru ya kwanza bila kupoteza mchezo, Yanga imedhamiria kuendeleza ubabe huo katika duru ya pili wakianza na Kagera Sugar leo

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kwani Kagera Sugar imeimarika sana ikiwa na mwenendo mzuri katika mechi za hivi karibuni

Kama Yanga itafanikiwa kuibuka na ushindi, itazidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya watani zao Simba ambao watashuka uwanjani March 03 kuikabili Biashara United

Katika mchezo wa leo Yanga itamkosa kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye ana kadi tatu za njano

Pia wataendelea kumkosa mlinzi Dickson Job ambaye leo anamaliza adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu

Kwa upande wa majeruhi, Jesus Moloko, Kibwana Shomari, Chrispine Ngushi, Yacouba Songne, Abdallah Shaibu na David Bryson wanaendelea kukosekana

Yassin Mustafa na Chico Ushindi wameimarika na pengine leo wanaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Kagera Sugar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’