Tunahitaji kufanya vizuri zaidi duru ya pili - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Feb 2022
Tunahitaji kufanya vizuri zaidi duru ya pili - Kaze

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedrick Kaze amesema wanahitaji kupambana katika duru ya pili katika ligi kuu ya NBC kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi walivyomaliza duru ya kwanza

Yanga imekamilisha mechi za mzunguuko wa kwanza pasipo kupoteza mchezo, wakishinda michezo 12 na kutoka sare michezo mitatu, wamefikisha alama 39 wakiongoza ligi kwa tofauti ya alama nane

Walikamilisha mchezo wa mwisho kibabe kwa kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Manungu Complex

Kaze amesema kwao hawafikirii nini wamefanya kwenye duru ya kwanza kwani matokeo hayo hayatakuwa na maana kama watashindwa kutimiza malengo waliyojiwekea ambayo ni kutwaa ubingwa

"Sitazungumza kuhusu rekodi za raundi ya kwanza ya ligi kwa sababu sio muhimu. Hata ukiwa na rekodi nzuri sana katika raundi ya kwanza, haitakuwa na maana kama mwishoni mwa ligi hutashinda vikombe," alisema Kaze

Yanga itaanza mechi za raundi ya pili Jumapili, Februari 27 kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
44m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’