Matchday Mtibwa Sugar vs Yanga, Manungu Stadium

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Feb 2022
Matchday Mtibwa Sugar vs Yanga, Manungu Stadium

Vinara wa ligi kuu ya NBC, Yanga Sc wako mkoani Morogoro ambapo jioni ya leo watashuka kunako dimba la Manungu kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa kukamilisha mzunguuko wa kwanza

Ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kushinda ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi wanayoongoza kwa tofauti ya alama tano baada ya kujikusanyia alama 36 kutoka michezo 14

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kwa Yanga hata kidogo, Mtibwa Sugar wamekuwa na mwenendo mzuri katika michezo waliyocheza katika uwanja wao wa Manungu ambao unachukua takribani mashabiki 2,500 tu

Mtibwa Sugar pia hawako katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi wakishika nafasi ya 15 wakiwa wamekusanya alama 12 kutoka michezo 14

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanafahamu ugumu wa mchezo huo lakini hakuna mchezo mwepesi waliocheza msimu huu. Hivyo wachezaji wanapaswa kupambana ili kuzipata alama tatu, hazitakuja zenyewe

Habari njema kwa Yanga ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi

Salum Abubakar 'Sure Boy', Kibwana Shomari na Denis Nkane wako tayari kuelekea mchezo huo wakiungana na Djuma Shabani ambaye amerejea baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu

Wachezaji watakaokosekana leo ni pamoja na Dickson Job anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, atakosa mchezo wa pili leo, Abdallah Shaibu 'Ninja', Yassin Mustafa, Chico Ushindi, David Bryson na Jesus Moloko nao watakosekana kwa sababu ni majeruhi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’