Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea mkoani Morogoro leo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Mchezo huo wa kukamilisha duru ya kwanza, utapigwa uwanja wa Manungu, Turiani siku ya Jumatano, Februari 23 2022
Baada ya miaka 24 kupita, Yanga inarejea kucheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu
Vinara hao wa ligi kuu wamefanya maandalizi 'kabambe' kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ingawa matokeo yoyote hayataathiri kumaliza duru ya kwanza wakiwa wanaongoza ligi
ADVERTISE HERE