Juzi katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United ambao Yanga ilifanikiwa kushinda mabao 2-1 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo, kiungo mshambuliaji Farid Mussa alitumika katika nafasi ya ulinzi upande wa kushoto
Ni baada ya Yanga kukumbwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi ambapo wachezaji 10 walikosekana
Hakukuwa na mlinzi wa upande wa kushoto baada ya Kibwana Shomari, David Bryson na Yassin Mustafa wote kuwa majeruhi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alianza kumjaribu Farid nafasi ya ulinzi wa kushoto katika mchezo wa kiarfiki dhidi ya Mbuni Fc mkoani Arusha
Kisha akamtumia kwa dakika chache kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City baada ya Bryson kuumia na kumtumia kwa dakika zote 90 kwenye mchezo dhidi ya Biashara United
Farid alionyesha umahiri mkubwa katika kushambulia na kuchezesha timu katika nafasi yake
Zipo nyakati lijisahau katika majukumu ya ulinzi lakini kama Nabi ataendelea kumtumia huenda akawa mlinzi mzuri wa kushoto
Ubora ambao alionyesha kwenye mchezo dhidi ya Biashara United unaweza kudhani Farid amekuwa akicheza nafasi hiyo kwa muda mrefu
Farid amedhihirisha kuwa mchezaji mwingine kiraka ambaye anaweza kutumika katika maeneo tofauti uwanjani
Kwani pamoja na kutumika katika nafasi ya winga, lakini pia zipo nyakati Nabi hupendekea kumtumia eneo la kiungo