Leo majira ya saa moja usiku Wananchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Biashara United katika mchezo wa raundi ya tano kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Ni mchezo muhimu kwa Yanga kwani matokeo ya ushindi yatawahakikishia kutinga robo fainali ya michuano hiyo
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema katika mchezo huo watawakosa wachezaji watano kutokana na sababu mbalimbali
Wachezaji ambao bado ni majeruhi ni David Bryson, Yassin Mustafa na Denis Nkane wakati Djuma Shabani leo anakosa mchezo wa tatu kumaliza adhabu yake ya kufungiwa
Dickson Job yeye leo anaanza kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu
Aidha Manara amesema kiungo Salum Abubakar nae hatma yake itategemea na utimamu wake baada ya mazoezi ya mwisho yaliyofanyika jana jioni
Katika hatua nyingine Manara amewataka mashabiki wa Yanga wasifanye vurugu za aina yoyote dhidi ya mashabiki wa timu nyingine watakaofika kushuhudia mchezo huo
Pamoja na kulaani tukio la mashabiki wa Simba kuwashambulia wa Yanga katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Asec Mimosas, Manara amesema kisasi na uadui sio sehemu ya utamaduni katika mpira wa miguu