Benchi la ufundi kufanyia kazi safu ya ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2018
Benchi la ufundi kufanyia kazi safu ya ushambuliaji
Kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini leo kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 15 dhidi ya Azam FC.

Juzi Yanga ilipata ushindi 'kiduchu' wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kupanda hadi nafasi ya tatu kwanye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 25.

Juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari, Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa alisema tatizo pekee linaloikabili Yanga kwa sasa ni ubutu wa safu ya ushambuliaji.

Nsajigwa alisema benchi la ufundi litahakikisha linaondoa tatizo hilo ili kuirejesha Yanga kwenye uwezo wake wa kufunga mabao mengi kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC

Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib ndio vinara wa upachikaji mabao katika kikosi cha Yanga wakiwa wamefunga jumla ya mabao 11.

Wawili hao walitengeneza pacha hatari lakini mwendelezo wake ulikatika baada ya Chirwa kuanza 'mgomo baridi' huku Ajib akikosekana kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Baadae Chirwa alifungiwa michezo mitatu na TFF kutokana na utovu wa nidhamu lakini sasa amemaliza adhabu hiyo.

Pengine kurejea kwa Chirwa kutarejesha makali ya upachikaji mabao ya kikosi cha Yanga.

Amissi Tambwe amekuwa majeruhi kwa muda mrefu. Tangu arejee dimbani hajafanikiwa kuzifumania nyavu kwenye ligi, pengine atahitaji muda zaidi kurejesha uwezo wake wa kuzifumania nyavu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’