Jana Waziri wa fedha Mh Mwigulu Nchemba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, aliweka bayana kusudio la Serikali kuboresha viwanja na zaidi uwezekano wa kuleta mfumo wa VAR kutokana na mfululizo wa makosa ya waamuzi
Kwa hakika huu utakuwa uamuzi sahihi na wenye manufaa ili kulinda hadhi ya ligi yetu ambayo sasa ni miongoni mwa ligi 10 bora barani Afrika
Matukio haya yameendelea kutokea na sasa inatia mashaka pale unapoona timu moja inaweza kunufaika kila wakati

Mijadala imekuwa mingi lakini haiwezi kumaliza tatizo hili bila ya mamlaka kuchukua hatua
Nafikiri sasa ni wakati wa mamlaka za usimamizi wa soka nchini kwa kushirikiana na Serikali kuchukua hatua
Katika ligi ya msimu huu wadhamini wameweka fedha nyingi na hilo limeongeza ushindani
Sasa uwekezaji huo hautakuwa na maana kama bado waamuzi watashindwa kutoa haki sawa kwa timu zote
Yapo matukio unaweza kusema waamuzi wanafanya makosa ya kibinadamu lakini kuna matukio ya dhadhiri shahiri ambayo waamuzi wanafanya makusudi
Jambo hili lipatiwe ufumbuzi haraka kwani uvumilivu huu wa mashabiki wa soka ukifika mwisho kuna siku yatatokea maafa