Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga leo watakuwa na nafasi ya kujikita zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi pale watakapowakaribisha Mbeya City katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa moja usiku
Ni msimu ambao Wananchi wanautaka kwelikweli ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu minne
Ili kutimiza malengo, ushindi katika michezo migumu ni matokeo muhimu zaidi
Mbeya City wamekuja jijini Dar es salaam kushindana na Yanga, timu hiyo iko ndani ya jiji kwa takribani wiki mbili wakiwa wamejichimbia huko Chamazi
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanatarajia mchezo wenye ushindani lakini wako tayari kuzisaka alama tatu
Katika mchezo wa leo Wananchi wanaweza kumshuhudia kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' aliyerejea kikosini baada ya kupona majeraha
Kulikuwa na hofu mlinzi Dickson Job kukosekana baada ya kuumia mazoezini, lakini Job alishiriki vyema mazoezi ya mwisho siku ya jana
Mlinda lango Djigui Diarra pia amerejea, benchi la ufundi kuamua nani aanze leo, Aboutwalib Mshery ameonyesha kiwango bora katika kipindi chote ambacho Diarra alikosekana
Khalid Aucho amemaliza adhabu ya kadi tatu za njano, anatarajiwa kurejea dimbani huku Shabani Djuma akiendelea kukosekana akitumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu
Atamaliza adhabu hiyo kwa kukosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United, Februari 15
Ni mchezo ambao wachezaji wa Yanga wanautaka kwelikweli na wamedhamiria kuondoka na alama zote tatu