Wakati wachezaji Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu 'Ninja' wakitarajiwa kurejea dimbani wakati wowote, mshambuliaji Yacouba Songne nae anaweza kurejea mapema kabla ya msimu huu kumalizika
Kibwana na Shaibu walifanyiwa upasuaji mdogo wa goti nchini Tunisia wiki mbili zilizopita, walisharejea nchini na kuanza mazoezi mepesi
Yacouba alifanyiwa upasuaji mkubwa wa goti ambao ulitarajiwa kumuweka nje ya uwanja wa miezi mitano
Hata hivyo Yacouba amekuwa na mwenendo mzuri wa uponaji akiwa anaendelea na program maalum ya mazoezi ya Gym

Pengine Wananchi wanaweza kumshuhudia akirejea uwanjani karibuni kunogesha mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu na kombe la FA
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alilazimika kumsajili winga Chico Ushindi baada ya Yacouba kuonekana kama hataweza kurejea uwanjani msimu huu