Jana Yanga imeichapa Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo ambao kama washambuliaji wa Ruvu wangekuwa makini wangeweza kuibuka na ushindi.
Licha ya ushindi huo, mashabiki wa Yanga wametoa maoni yao wengi wakisikitishwa na kiwango kisichoridhisha kilichoonyeshwa na wachezaji.
Wengi wanahofia kama hakutakuwa na mabadiliko, mchezo ujao dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu zaidi kwa Yanga.
Yanga itaivaa Azam FC Jumamosi ijayo, Januari 27 kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Azam FC haijapoteza mchezo wowote msimu huu na imekuwa haifungiki(kwa mujibu wa takwimu) inapocheza kwenye uwanja wake wa Chamazi.
Jana imeilaza Prisons mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mkoani Mbeya. Pia hawa ndio mabingwa wa kombe la Mapinduzi walilotwaa wiki iliyopita visiwani Zanzibar.
Yanga itahitaji kuwa kwenye kiwango bora kukabiliana na wauza ice cream hao.
Hata hivyo Yanga itapata ahueni kwenye mchezo huo kwa baadhi ya wachezaji wake Kelvin Yondani na Obrey Chirwa kurejea kikosini.
Yondani alikosa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano huku Chirwa akiwa amemaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu kutokana na utovu wa nidhamu.
Huenda pia kiungo Thabani Kamusoko akawa tayari kurejea dimbani kwenye mchezo huo.

ADVERTISE HERE