Kikosi cha Yanga kiko jijini Mwanza ambapo jioni ya leo watashuka katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao Fc katika mchezo wa raundi ya nne kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Vinara hao wa ligi kuu ya NBC wanahitaji ushindi ili kutinga hatua ya 16 bora
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo anatarajiwa kufanya mabadiliko ya kikosi chake kutokana na kuwakosa baadhi ya wachezaji
Takribani nyota sita wa kikosi cha kwanza hawatakuwa sehemu ya mchezo huo
Mlinda lango Djigui Diarra ambaye alikuwa Cameroon kushiriki michuano ya Afcon akiwa na kikosi cha Mali, bado hajarejea nchini baada ya Mali kuondoshwa katika michuano hiyo
Walinzi Yannick Bangala na Djuma Shabani wako katika majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo. Djuma pia anatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu
Kiungo Khalid Aucho anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano wakati Feisal Salum 'Fei Toto' bado hajarejea katika utimamu wake kwa asilimia 100 baada ya kupata majeraha
Heritier Makambo pia hatakuwa sehemu ya mchezo huo pamoja na kocha msaidizi Cedric Kaze ambao wana matatizo ya kifamilia
Hata hivyo kukosekana kwa nyota hao haliwezi kuwa tatizo kwa Nabi kwani anao watu wa kazi wanaoweza kuihakikishia Yanga ushindi