Mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya Mbao Fc ambao umepangwa kupigwa Jumamosi, Januari 29, utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba
Baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa ambao ulipaswa mchezo huo kupigwa kuwa na matumizi mengine siku ya Jumamosi, Yanga imeomba mchezo huo ukapigwe CCM Kirumba na TFF wameridhia ombi hilo
Wananchi wa Mwanza hii ni nafasi yenu kuishuhudia timu yenu kwa mara ya kwanza msimu huu

ADVERTISE HERE