Bacca, Ushindi wataongeza ubora Yanga - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2022
Bacca, Ushindi wataongeza ubora Yanga - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameeleza kuridhishwa na viwango vilivyoonyeshwa na nyota wapya, beki Ibrahim Bacca na mshambuliaji Chico Ushindi ambao walifunga usajili wa Yanga katika dirisha dogo

Nabi amesema wachezaji hao wameonyesha viwango vizuri licha ya kuwa bado hawako katika utimamu anaotaka

"Bacca ni mchezaji mzuri tuliyemsajili kutoka Zanzibar na Chico Ushindi amejiunga nasi akitoka TP Mazembe"

"Hawa ni wachezaji wazuri na wameonyesha uwezo wao. Bado hawako katika utimamu tunaotaka, watakapokuwa tayari wataongeza kitu katika timu yetu," alisema Nabi

Katika hatua nyingine Nabi amesema wataendelea kujipanga kuhakikisha wanashinda mechi zao ili kuweza kutimiza malengo

Pamoja na Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 10, Nabi amesema hiyo sio muhimu sana kwao, wanaangalia mbele kuhakikisha wanaendelea kushinda mechi zijazo

Yanga imerejea jijini Dar es salaam leo wakitokea Arusha ambapo jana walifanikiwa kuondoka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania

Yanga inajiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa Jumamosi, Januari 29 2022

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’