FT : Yanga 2-0 Mbuni Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jan 2022
FT : Yanga 2-0 Mbuni Fc

Yanga imewachakaza vinara wa ligi kuu ya Daraja la pili Mbuni Fc mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha

Mabao yote ya Yanga yalifungwa na Mukoko Tonombe 'Teacher' kupitia mikwaju ya penati

Penati ya kwanza alifunga kwenye dakika ya 56 baada ya mlinzi wa Mbuni Fc kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Penati ya pili alifunga kwenye dakika ya 80 baada ya winga mpya aliyetua juzi kutoka TP Mazembe, Chico Ushindi kuangushwa ndani ya eneo la hatari

Ulikuwa ni mchezo ambao kwa upande mwingine mazoezi kwa wachezaji wa Yanga wanaojiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa uwanja wa Ushirika, Jumapili

Leo mashabiki wa Yanga wamemshuhudia mlinzi mpya wa timu Bacca aliyeng'ara kwenye safu ya ulinzi akianza sambamba na Mukoko

Crispine Ngushi ndiye aliyesababisha mkwaju wa kwanza wa penati huku Sure Boy, Zawadi Mauya na Mapinduzi Balama wakitakata kwenye eneo la kiungo

Balama ameendelea kuimarika baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja

Ushindi ameanza vyema maisha yake na Yanga kwani mchezo wake wa kwanza ameonyesha ni mchezaji hatari akisababisha mkwaju wa penati pia

Mbuni Fc walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mlinzi wao kumkanyanga mgongoni David Bryson na kutokewa nje kwa kadi nyekundu

Bryson alishindwa kuendelea na mchezo huo ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Ngushi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’