Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa mshambuliaji wa Yanga, Yacouba Songne
Yacouba yuko nje ya dimba akiunguza majeraha ambayo yatamuweka nje mpaka msimu ujao
Mfungaji bora huyo wa kikosi cha Yanga katika msimu uliopita, kukosekana kwake sio pigo tu kwa Yanga, bali hata kwa timu yake ya Taifa Burkina Faso ambayo inashiriki michuano ya Afcon 2021 huko Cameroon
Pengine Yacouba jana angekuwa sehemu ya kikosi cha Burkina Faso kilichocheza na Cameroon kwenye mchezo wa ufunguzi michuano ya Afcon ambao ulimalizika kwa wenyeji kushinda mabao 2-1
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii muhimu kwake
HAPPY BIRTHDAY YACOUBA...!
ADVERTISE HERE