Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taifa ya Jan'gombe hapo jana, Yanga inakamilisha ratiba ya hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Mapinduzi kwa kuikabili KMKM katika mchezo utakaopigwa Ijumaa, January 07 katika uwanja wa Amaan
Mtanange huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali, utapigwa kuanzia saa kumi na robo jioni
KMKM ndio vinara wa ligi kuu ya Zanzibar, wakiwa na msimu mzuri mpaka sasa
Katika mchezo wa kesho kikosi cha Yanga kitaongezewa nguvu na wachezaji waliowasili leo ambao walikuwa mapumziko
ADVERTISE HERE