Djuma Shabani, Mukoko Tonombe na Yannick Bangala wameondoka nchini leo kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya DR Congo iliyoweka kambi huko Arabuni
Nyota hao ni miongoni mwa wachezaji 23 wanaojiandaa na mchezo wa play-off kusaka tiketi ya michuano ya kombe la Dunia
Wanaungana na mlinda lango Djigui Diarra ambaye yuko Cameroon kushiriki michuano ya Afcon 2021 na timu ya Taifa ya Mali
Yanga itawakosa wachezaji hao kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi pamoja na nyota wengine ambao Kocha Nasreddine Nabi anaweza kuwapumzisha baada ya kutumika sana
ADVERTISE HERE