Matokeo dhidi ya Mwadui FC yametusikitisha - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
18 Jan 2018
Matokeo dhidi ya Mwadui FC yametusikitisha - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema benchi la ufundi halifurahishwi na matokeo ya mchezo dhidi ya Mwadui FC.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo jana, Nsajigwa amesema Yanga ilihitaji kupata ushindi katika mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne.

Hata hivyo amesema mbinu za kujilinda zilizotumiwa na Mwadui FC ziliinyima Yanga ushindi.

“Matokeo kwetu sio mazuri kwa sababu malengo yetu ni kutetea ubingwa, tulihitaji sana hizi pointi tatu za leo angalau tupunguze idadi ya pointi ambazo wenzetu wametutangulia, tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu lakini bahati mbaya tumeshindwa kupata pointi tatu ingawa tupo kwenye uwanja wa nyumbani.”

“Niwapongeze Mwadui kwakuwa wamefanya vizuri homework yao, mwanzo tulikuwa tunacheza kama wanavyocheza wao lakini baadaye tukabadilisha tukaanza kutumia mipira mirefu lakini njia zote waliziba.”

“Tukaamua kucheza kwa kutumia pembeni lakini bado hatukuwa na nguvu nzuri ya kwenda kumalizia magoli kwa hiyo niwapongeze Mwadui kwa walichokifanya, walicheza vizuri wamepata pointi moja,” amefunguka Nsajigwa

Baada ya mchezo huo Yanga inajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shoooting, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jumapili, Januari 21 2018
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →