Huyo Zawadi Mauya anauwasha moto hatari! Jana alionyesha kiwango bora sana kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United ambao Yanga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1
Katika mchezo huo kiungo mpya wa Yanga Salum Abubakari 'Sure Boy' alikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo ambao alipata nafasi ya kusalimia mashabiki wakati wa mapumziko
Itoshe kusema kwa sasa Yanga ndio timu yenye safu bora ya kiungo katika ligi kuu ya NBC
Kocha Nasreddine Nabi ana watu wa mpira kwelikweli katika eneo hilo
Anaweza kuanza na Khalid Aucho, Yannick Bangala na Feisal Salum lakini pia anaye Mauya, Sureboy na Mukoko Tonombe


Ukiacha ubora wa safu ya kiungo, hata maeneo mengine yamekamilika, safu ya ulinzi na ushambuliaji pia
Yanga inafunga mabao kutoka kila eneo, Mayele ana mabao manne, Feisal ana mabao manne, Saido ana mabao matatu, Jesus Moloko ana mabao mawili
Djuma Shabani, Mukoko na Khalid Aucho nao wamefunga pia
Wananchi hawategemei mchezaji mmoja kufunga mabao