Wananchi wamefanikiwa kuondoka na alama zote tatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United
Ulikuwa mchezo mgumu ambao Yanga ililazimika kutokea nyuma kupata ushindi huo muhimu
Bao la dakika ya pili lililofungwa na Atupele Green liliiweka Yanga katika presha kubwa ya kusaka bao la kusawazisha kwa karibu kipindi chote cha kwanza
Yalikuwa ni makosa ya mlinda lango Djigui Diarra ambaye alishindwa kuweka kwenye himili yake mpira wa krosi
Fiston Mayele aliirejesha Yanga mchezo kabla ya mapumziko kwa bao safi ya tikitaka akimalizia krosi ya Djuma Shabani

Yanga ilitawala mchezo huo kwa pasi nyngi lakini Biashara United walikuwa hatari kupitia mashambulizi ya kushitukiza
Kasi ya Jesus Moloko iliinufaisha Yanga kwenye dakika ya 79 baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kutoa mkwaju wa penati
Saido Ntibazonkiza akafunga mkwaju huo na kuihakikishia Yanga kuondoka na alama zote tatu
Wananchi wameendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 26