Baada ya shamrashamra za Sikukuu ya Christmas, mshike mshike wa ligi kuu ya NBC unaendelea leo ambapo vinara wa ligi, Yanga watakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Biashara United
Ni 'Boxing Day', siku ya kufungua zawadi, Yanga ikipania kupendezesha siku hii kwa kuibuka na ushindi
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja jioni yamekamilika ambapo amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao
Akizungumzia hali ya kikosi, Bumbuli amesema hakuna majeruhi wapya zaidi ya Kibwana Shomari, Yusufu Athumani na Yacouba Songne
Kiraka Yannick Bangala ambaye alikosa mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kuugua homa na mafua, yuko tayari kurejea uwanjani
Ni mchezo mwingine ambao Yanga inahitaji mkushinda ili kuendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Yanga imejihakikishia kufunga mwaka 2021 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 23 kutoka michezo 9