Kwa mujibu wa takwimu, Feisal Salum 'Fei Toto' ndiye mchezaji hatari zaidi ambaye timu pinzani hazitamani kukutana nae wakati huu
Katika michezo tisa, amefunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao
Huyu ni mchezaji ambaye Emmanuel Amunike, aliyewahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' alikiona kipaji chake na hata kubainisha kuwa alikuwa na uwezo wa kucheza hata katika klabu kubwa kama Fc Barcelona
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alifanya tathmini yake vema na kubaini eneo ambalo anaweza kumtumia Fei Toto kwa mafanikio, leo anafunga, anatoa usaidizi katika kupatikana mabao
Kama Mzambia Clatous Chama angekuwa bado yuko Tanzania na kuwa na takwimu kama za Feisal alizonazo katika mechi tisa msimu huu, vipindi vya michezo na wachambuzi huko mitandao wangekuwa wakijaza kurasa zao kwa kumsifia kuwa mchezaji bora
Ni ajabu sana! lakini ndivyo tulivyo Watanzania, hatupendi kuthamini vya kwetu. Wanayanga wana kila sababu ya kujivunia Feisal, huyu ndiye mchezaji bora katika ardhi ya Tanzania kwa sasa