Sure Boy kaweka ngumu kurudi Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Dec 2021
Sure Boy kaweka ngumu kurudi Azam Fc

Baada ya uongozi wa Azam Fc kutangaza kuwasamehe nyota wao Salum Abubakari 'Sure Boy', Aggrey Morris na Mudathir Yahya na kuwataka warejee kikosini, Sure Boy amesisitiza kutorejea katika klabu hiyo huku akitaka kuvunja mkataba wake

Azam Fc iliwasimamisha wachezaji hao kwa muda usiojulikana wakituhumiwa na makosa ya utovu wa nidhamu,  ikatangaza kuwasamehe baada ya kuibuka tetesi kuwa nyota hao wanahitajiwa na klabu za Yanga na Simba

Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zakaria 'Zakazakazi' amethibitisha kuwa Mudathir na Morris wamerejea kikosini lakini Sureboy amewasilisha maombi ya kuvunja mkataba wake

"Sure Boy yeye hajaungana na wenzake na ameomba kwa mdomo kuvunja mkataba baada ya kuitumikia Azam kwa muda mrefu. Tunasubiri barua rasmi kutoka kwake," alisema Zakazakazi

Je baada ya majaribio ya Yanga kumn'goa Sure Boy Azam Fc kwa misimu kadhaa kugonga mwamba, safari hii itawezekana?

Msimu uliopita ilibaki kidogo tu Yanga imsajili lakini Azam Fc wakapindua meza dakika za majeruhi na kufanikiwa kumbakisha huku wakimuongezea mkataba wa mwaka mmoja

Mgogoro ulioibuka karibuni pengine unaweza kuinufaisha Yanga kumnasa nyota huyo ambaye anataka kufuata nyayo za Baba yake Abubakar Salum 'Sure Boy OG' ambaye aliitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa

Sure Boy ameonyesha hataki tena kuitumikia Azam Fc hasa baada ya kusimamishwa katika mazingira ya kutatanisha na kusamehewa baada tetesi kumuhusisha na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’