Klabu ya Azam Fc imewaruhusu nyota watatu wa timu hiyo waliosimamishwa kusaka timu baada ya kutokuwa na mpango wa kuwarejesha kikosini
Salum Abubakar 'Sure Boy', Mudathir Yahya na Aggrey Morrison walisimamishwa na Azam Fc kwa muda usiojulikana wakituhumiwa na makosa ya utovu wa nidhamu
Imeelezwa Yanga iko katika hatua za mwisho kumsajili Sure Boy, mchezaji waliyemuwania kwa misimu kadhaa bila ya mafanikio
Kama Yanga itakamilisha usajili huo, basi watakuwa wameongeza mchezaji mahiri sana katika eneo la kiungo
Wananchi pia wanatajwa kuiwania saini ya winga hatari wa Biashara United Denis Nkane
Nkane amekuwa na kiwango bora sana katika kikosi cha Biashara United
Kinda huyo anamudu kucheza nafasi zote za ushambuliaji akitokea pembeni
Nkane ni kijana mdogo anayefananishwa na Mrisho Ngasa, nyota aliyewahi kutamba na kikosi cha Yanga na timu ya Taifa