Mwaka 2021 unaelekea ukingoni ambapo kikosi cha Yanga kinatarajiwa kukamilisha mwaka huu kwa kucheza mechi nne katika kipindi cha siku 15
Jumatano, Disemba 15 Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ihefu Fc katika mchezo wa raundi ya tatu michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Baada ya mchezo huo Wananchi watasafiri mkoani Rukwa, ambapo Disemba 19 wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Nelson Mandela, moja ya viwanja vigumu kuondoka na alama tatu
Yanga itafunga mwaka kwa michezo yake miwili ya mwisho kupigwa jijini Dar es salaam ambapo Disemba 26 watacheza na Biashara United uwanja wa Benjamin Mkapa na kufunga mwaka 2021 kwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Disemba 31
Wananchi wakiwa na malengo ya kushinda ubingwa msimu huu, ni mechi ambazo wanapaswa kuondoka na alama zote tatu licha ya kuwa itakuwa michezo migumu