Profesa Nabi, ni siku nyingine kudhihirisha ubora wake kimbinu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2021
Profesa Nabi, ni siku nyingine kudhihirisha ubora wake kimbinu

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo anakwenda kuwaongoza wananchi katika mchezo wa nne dhidi ya Simba

Nabi aliyetua Yanga mwezi April, katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya Simba, ameshinda michezo miwili, na kupoteza mchezo mmoja

Ushindi wake wa kwanza dhidi ya Simba ilikuwa Julai 03 katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita, Wananchi wakiondoka na ushindi wa bao 1-0

Akapoteza mchezo wa pili uliokuwa wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) mkoani Kigoma

Kuelekea msimu huu, Nabi akashinda mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ulipigwa Septemba 25

Nabi tayari anaifahamu presha ya dabi hivyo kwake mchezo wa leo anajua ni vipi apange kikosi chake kuhakikisha anaibuka na ushindi

Tayari anacho kikosi cha kwanza, mabadiliko ya lazima ni kwa nafasi ya Yacouba Songne ambaye ni majeruhi

Mkongwe Saido Ntibazonkiza ametumika katika michezo miwili iliyopita na akafanikiwa kufunga mabao mawili

Leo Ntibazonkiza anatarajiwa kuanza huku Farid Mussa na Deus Kaseke wakiwa tayari kama Nabi atawahitaji

Ni mchezo ambao presha itakuwa kubwa zaidi kwa kocha wa Simba Pablo Franco ambaye ni mchezo wa kwanza wa dabi kwake

Kwa Nabi leo ni siku nyingine kwake kudhihirisha ubora wake kimbinu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’