Mayele ni hatari, Makambo sio mbaya - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2021
Mayele ni hatari, Makambo sio mbaya - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema mshambuliaji Fiston Mayele anastahili kuanza katika kikosi cha kwanza mbele ya Heritier Makambo kutokana na ubora anaoonyesha uwanjani

Makambo ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Yanga, amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi katika mechi saba za ligi ambazo Yanga imecheza mpaka sasa

Hata hivyo hakuna shabiki anayeweza kuhoji uamuzi wa Nabi kumtumia Mayele kama mshambuliaji wake namba moja

Mayele amepachika mabao matatu katika mechi saba za ligi huku akitoa pasi moja ya bao. Ameonyesha uwezo mkubwa sana akiwa mwiba mkali kwa walinzi wa timu pinzani

Nabi amesema anajivunia kuwa na washambuliaji hao wawili katika kikosi chake kwani hata Makambo nae sio mshambuliaji mbaya

Lakini amesisitiza sio rahisi kwa kocha kumuweka nje mchezaji ambaye yuko kwenye ubora, akifanya kazi yake vyema

"Mashabiki wanampenda Mayele na anafanya vizuri sana akiwa uwanjani, mimi kama kocha siwezi kumweka nje mchezaji ambaye anafanya kazi nzuri uwanjani.

"Wapo wanaohoji kwa nini Makambo hachezi, siyo mchezaji mbaya anaonyesha jitihada kubwa sana kwenye uwanja wa mazoezi. Nafikiri atapata nafasi kulingana na mahitaji ya mechi," alisema Nabi

Kumekuwa na tetesi kuwa Makambo hafurahii kutopata nafasi kikosini ikielezwa kuwa klabu ya AS Vita imeonyesha nia ya kutaka kumsajili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’