Ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Mbeya Kwanza mapema wiki hii umewafanya Wananchi wazidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 19
Aidha Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi zaidi msimu huu ikiwa imeweka kambani mabao 12 na kuruhusu mabao mawili kutikisa nyavu zake
Mlinda lango Djigui Diarra ana 'cleansheet' tano katika michezo saba aliyokaa kulinda lango la Yanga
Fiston Mayele na Feisal Salum ndio vinara wa kufunga mabao katika kikosi cha Yanga kila mmoja akiweka kambani mabao matatu
Jesus Moloko na Saido Ntibazonkiza wao wamefunga mabao mawili kila mmoja wakati Shabani Djuma na Mukoko Tonombe kila mmoja amefunga bao moja
Ni mwanzo mzuri wa msimu kwa Yanga ambayo imepania kushinda ubingwa wa ligi kuu ya NBC msimu huu