Nabi amkubali Kaze, asema mambo bado

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2021
Nabi amkubali Kaze, asema mambo bado

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Mohammed Nabi amemuhakikishia Mwenyekiti wa kamati ya ufundi Dominick Albinus kuwa watakuwa na timu bora zaidi ya hii ya sasa kadiri wanavyoendelea kukiimarisha kikosi

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza, Albinus hakusita kumpongeza Nabi kwa mchezo mzuri wa kikosi chake ambao umewahakikishia kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukusanya alama 19

"Sikiliza nikwambie kitu Mwenyekiti, hii timu unayoona leo inacheza vizuri na kupata matokeo siyo timu iliyokuwa kichwani kwangu,hapa tulipo bado tunacheza kwa asilimia 60 tu ya ile timu yangu ya Yanga iliyoko kichwani," alisema Nabi

Aidha kocha huyo mwenye uraia pacha wa Tunisia na Ufaransa, amesema anapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Kocha Msaidizi Cedric Kaze ambaye anafanya kazi kubwa usiku na mchana kuhakikisha wanatimiza mipango yao kwenye viwanja vya mazoezi

"Hapa tulipo tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa sana na wasaidizi wangu katika benchi la ufundi ili tuweze angalau kupenyeza ujuzi wetu wakati ligi ikiendelea na hilo tunalifanya kwa umakini sana ili kutowachanganya wachezaji kwani wapo katika mashindano"

"Kaze amekuwa msaada mkubwa sana kwangu kwani tumekuwa tukisaidiana katika kukamilisha mipango yetu ya mazoezi na ufundi kwa kikosi chetu ili tufikie malengo ya ubingwa"

"Kaze pia ni mwalimu makini na mchapakazi ambaye amekuwa akifanya kazi ionekane kuwa rahisi kwani ni kocha wa kiwango cha juu. Kuunganisha kwetu nguvu kutaleta matunda na faida kubwa sana kwa kikosi hiki na hakika muda sio mrefu tutakuwa na timu tishio Afrika"

Nabi amesema kuwa baada ya mwezi mmoja yaani kuanzia Januari timu itakuwa inacheza angalau kwa asilimia 80 ya timu anayoitaka kwani ikumbukwe kuwa hakupata maandalizi ya kutosha ya kulekelea msimu huu kutokana na changamoto mbalimbali hivyo wao kama benchi la ufundi wanaendelea kufanya vyote kwa wakati mmoja

"Hatukupata pre-season hapo awali hivyo inatibidi sisi kama benchi la ufundi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja ambayo ni kuwaweka wachezaji kwenye utimamu wa miili pamoja na kuwapa mbinu tofauti tofauti za kupambana na timu tofauti"

"Kwasasa tunakwenda kuanza maandalizi ya kuelekea mchezo unaokuja,waambie wanayanga wawe na subira mambo mazuri yanakuja muda sio mrefu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’