Kiungo fundi wa Yanga Khalid Aucho jana alijumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi yanayoendelea Avic Town, Kigamboni
Aucho alirejea nchini juzi akitokea kwao Uganda alikokuwa akiuguza majeraha aliyopata wakati akiwa na timu ya Taifa
Kurejea kwake ni habari njema kwa Kocha Nasreddine Nabi ambaye anakiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya Kwanza ambao utapigwa Novemba 30 uwanja wa Sokoine, Mbeya
Aucho alikosa mechi mbili zilizopita dhidi ya Ruvu Shooting na Namungo Fc lakini hakuna shaka atakuwepo mkoani Mbeya
ADVERTISE HERE