Ni fainali nyingine kwa Yanga mkoani Mbeya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2021
Ni fainali nyingine kwa Yanga mkoani Mbeya

Kikosi cha Yanga kimeingia kambini jana kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya Kwanza ambao utapigwa Novemba 30 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya

Ni mchezo mwingine mgumu kwa Yanga, lakini muhimu sana kwa Wananchi kushinda hasa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopita

Mechi zote ambazo Yanga hucheza mkoani Mbeya huwa si nyepesi, moja ya mikoa migumu sana kwa Yanga kuondoka na alama tatu

Msimu uliopita Wananchi walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, mchezo ukigubikwa na matukio mengi yaliyopeleka lawama kwa waamuzi

Baada ya mazoezi ya jana jioni yaliyofanyika Avic Town, wachezaji waliingia kambini moja kwa moja kujiwinda na mchezo huo

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wana muda wa kutosha kujiandaa na watafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita

Katika mchezo dhidi ya Namungo, Nabi alitupia lawama uwanja wa Ilulu lakini sasa amesema anawaandaa vijana wake kupata matokeo katika uwanja wowote na kuwa wanapaswa kubadilika kimbinu kulingana na changamoto wanazkutana nazo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’