Tanzania imehitimisha kampeni ya kusaka tiketi ya michuano ya kombe la Dunia nchini Madagascar kwa kupata alama moja ugenini baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1
Simon Msuva alifunga bao pekee la Tanzania kwenye kipindi cha kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Feisal Salum 'Fei Toto'
Ulikuwa mchezo mgumu ambao wenyeji walionekana kujipanga kuanzia nje ya uwanja kupata ushindi
Walifanikiwa kusawazisha bao hilo kwenye kipindi cha pili, licha ya kushambulia lango la Tanzania kwa muda mwingi, hawakuweza kuongeza bao
Tanzania inamaliza katika nafasi ya tatu kundi J ikikusanya alama nane
DR Congo imetinga hatua ya mtoano baada ya kuichapa Benin mabao 2-0 na hivyo kufikisha alama 11
ADVERTISE HERE