Mpaka sasa tunaweza kusema mshambuliaji Fiston Mayele ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi ya Yanga katika mechi zote za mashindano na kirafiki
Jana Mayele alifunga bao lake la tisa msimu huu katika ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga waliupata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM
Katika michezo 14 ambayo alipata nafasi ya kuwemo katika kikosi cha Yanga, Mayele amefunga katika michezo tisa na kufanya usaidizi wa kupatikana mabao katika michezo mitatu
Hakika Mayele ni mshambuliaji hatari, hakuna shaka, msimu huu Mayele atakuwa chachu ya mafanikio ya kikosi cha Yanga
Baada ya kuteswa na eneo la ushambuliaji kwa misimu kadhaa, msimu huu tiba imepatikana!

ADVERTISE HERE