Tanzania imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya DR Congo
Ni matokeo ambayo hayakutarajiwa lakini, ndivyo ilivyokuwa hapo uwanja wa Benjamin Mkapa Wacongo wakiondoka na ushindi licha ya kutocheza vizuri kulinganisha na Tanzania
Walikuwa makini zaidi kwenye matumizi ya nafasi tofauti na Tanzania ambayo haikutumia nafasi nyingi walizotengeneza hasa kwenye kipindi cha kwanza
Tanzania imeondoshwa mashindanoni baada ya kipigo hicho huku Benin wakiongoza kundi J baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Madagascar
ADVERTISE HERE