Makambo apania kurejea upya kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2021
Makambo apania kurejea upya kikosini

Mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo ameapa kutumia kipindi hiki cha mapumziko ya michuano ya Kimataifa kujiimarisha ili kuhakikisha anarejea kwenye kikosi cha kwanza

Makambo amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kuanza mbele ya Mcongomani mwenzake Fiston Mayele ambaye ni 'wa moto' kwelikweli

Mshambuliaji huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga amefichua kuwa alifanya kikao na kocha Nasreddine Nabi ambapo amesema mazungumzo hayo yamemuongezea ari

"Ligi iliposimama nimepata nafasi ya kuongea na kocha pamoja na viongozi na kuna mambo tumezungumza ambayo rasmi yamenirudisha akili yangu katika soka na kufanya kile ambacho kinahitajika"

"Nimeanza mazoezi yangu binafsi katika wakati huu kabla ya yale ya timu ili kuimarika zaidi na tutakapokwenda mazoezini nitafanya vitu vilivyokuwa bora kwa kutimiza majukumu yangu pengine zaidi ya wakati wote," alisema Makambo

Makambo hakujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Azam Fc na Ruvu Shooting kutokana na kanuni inayoelekeza wachezaji nane wa kigeni kutumika katika mchezo mmoja

Saido Ntibazonkiza, Mukoko Tonombe na Makambo wamekuwa wakibadilishana nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha mechi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’