Yanga inaongozwa na Katiba yake GSM inasaidia tu - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2021
Yanga inaongozwa na Katiba yake GSM inasaidia tu - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said amesema mjadala ulioanzishwa na baadhi ya wachambuzi kuhusu udhamini wa kampuni ya GSM kwa vilabu mbalimbali ligi kuu ni siasa chafu kwa kuwa sio jambo geni katika ulimwengu wa soka

Akizungumza na EA Radio, Injinia Hersi amesema yapo makampuni makubwa duniani ambayo yanadhamini klabu nyingi tu na hakujawahi kuwa na mjadala wowote

"Watu wanaleta siasa chafu na mimi nasema hizi ni takataka. Mbona kampuni kama Emirates inadhamini vilabu vingi tu vinacheza Champions League. Ina maana Arsenal wakicheza na AC Milan utasema mmoja amwachie mwenzake?," alihoji Injinia Hersi

Aidha Hersi amesema wao katika klabu ya Yanga wanasaidia tu, timu inaongozwa kwa kufuata misingi na taratibu za klabu yenyewe na sio kufuata matakwa ya GSM

"Yanga inalipa mishahara yenyewe, ina mifumo yake ya kuajiri watu sisi tunasaidia tu. Yanga ni timu kubwa huwezi kufananisha na hawa makolo. Huwezi kumleta mchezaji kama Bangala halafu hajui mshahara analipwa na nani"

"Hii ni klabu kubwa, tunafanya kazi ya kurejesha heshima yake, watu waipende tena. Angalia mechi ya juzi Yanga inafungwa goli mashabiki wanapiga makofi, tunarudisha tunafunga la pili na la tatu na bado kuna dakika kama 900 za kucheza," aliongeza Hersi

Hersi pia aligusia mfumo wa uwekezaji ambao klabu ya Yanga imeamua kufuata baada ya kushauriwa na La Liga akiamini unakwenda kuinufaisha klabu hiyo

"Tumechagua mfumo wa wanachama na wawekezaji kwa 51% kwa wanachama na 49% kwa wawekezaji. Hili tumejifunza La Liga na ndio maana unaweza ukaona kwanini Real Madrid na Barcelona zinapendwa na watu duniani"

"Tumejifunza kitu kikubwa sana na mabadiliko ya Yanga yatakwenda kuwa ya mfano. Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
27m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’