Pamoja na ushindi mfululizo, Nabi anasema bado

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2021
Pamoja na ushindi mfululizo, Nabi anasema bado

Kocha Mkuu wa Yanga Nasriddine Nabi, amesema pamoja na ushindi mnono walioupata dhidi ya Ruvu Shooting, bado timu hiyo ipo katika kipindi cha mpito kuelekea kwenye ubora anaouhitaji

Yanga juzi iliandikisha ushindi wake wa tano mfululizo kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kwa kuifunga Ruvu Shooting ya Pwani mabao 3-1, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Nabi ameeleza kufurashishwa na maendeleo ya timu yake na zaidi kuona kile alichoahidi cha kupewa muda wa kuitengeneza timu hiyo kimeanza kuonesha matunda kwa ushindi wanaoupata, lakini bado ana kiu ya kuijenga zaidi timu hiyo.

"Nafurahi kuona tunacheza na kupata ushindi kwenye mechi zetu tano za ligi mchezo wa leo (juzi), ulikuwa mgumu. Ruvu ni timu nzuri siku zote huwa inajiandaa kucheza na timu kubwa, msimu uliopita tuliwafunga kwa tabu mabao 3-2, lakini pia waliifunga Simba bao 1-0, siyo wa kuwadharau," alisema Nabi

Kocha huyo raia wa Tunisia alisema matokeo wanayoyapata hivi sasa ni sehemu ya kile alichokiahidi wakati anakuja nchini kwamba anataka kutengeneza utambulisho halisi wa Yanga (DNA), kwa sababu ya ukubwa iliyonayo timu hiyo Afrika Mashariki

Alisema ingawa watu wameanza kuwafananisha na FC Barcelona kwa aina ya soka la pasi nyingi wanalocheza, lakini hakuna ukweli katika hilo, kwani Yanga itabaki kama Yanga kwa kucheza soka la aina anayotaka yeye hivi sasa

"Ninachotaka siyo kumfunga mpinzani mabao mengi, lakini pia tucheze soka la kuvutia lenye pasi nyingi lionekane kwa mashabiki, ambao wanajazana kwa wingi kuja kutupa sapoti na hilo linawezekana kwa mwenendo tuliokuwa nao, hivyo ikitimia miezi mitatu niliyoahidi watu watajionea" 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’