Faili la Malinzi latua TAKUKURU

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jan 2018
Faili la Malinzi latua TAKUKURU
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, DPP ametoa maagizo mapya kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kufanya marekebisho ya upelelezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake inayosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.

Malinzi anashitakiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka zikiwemo risiti 20 za TFF pamoja na shitaka la utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 375,418 akiwa na washitakiwa wengine ambao ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Nsiande Mwanga ambaye alikuwa muhasibu wa shirikisho hilo.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, upande wa mashitaka kupitia Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Leornad Swai, jana Alhamisi aliiambia mahakama kuwa tayari faili la Malinzi na wenzake lipo mikononi mwao baada ya kutoka kwa DPP ambaye ametoa maagizo mapya kwenye upelelezi wake.

Swai alidai kuwa faili hilo lipo mikononi mwa Takukuru kwa ajili ya kuendelea na upelelezi wa kesi hiyo baada ya kupokea maelekezo ya marekebisho kwenye upelelezi wa kesi hiyo kutoka kwa DPP, hivyo wanaomba wapangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa tena kesi hiyo.

Kutokana na hoja hiyo upande wa utetezi ambao ulikuwa ukiongozwa na mawakili, Abraham Senguji na Nehemia Nkoko haukuweza kupinga chochote kabla ya Hakimu Mashauri kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 25, mwaka huu.

Champion
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’